Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

TAARIFA KUTOKA TCAA KUHUSU KOZI YA URUBANI KATIKA CHUO CHA TANZANIA AVIATION UNIVERSITY COLLEGE (TAUC)


Hivi karibuni Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imebaini kuwa chuo cha Aviation University College (TAUC) kilichopo Tabata, Dares salaam, ambacho kimeidhinishwa na TCAA kutoa kozi ya maafisa wa kutoa huduma katika kampuni za ndege yaani Flight Operations Officers/Flight Dispatcher (FOO), kimekuwa kikiweka matangazo kuwa kinatoa kozi za urubani kwa ngazi ya PPL, taarifa ambazo sio sahihi.

TCAA imebaini suala hilo wakati ilipofanya ukaguzi  katika chuo hicho cha TAUC. Tayari TCAA imewasiliana na chuo cha TAUC ambacho kimeondoa tangazo hilo katika tovuti yake. 

Kwa taarifa hii, tunapenda kutahadharisha umma kuwa, chuo cha Tanzania Aviation University College (TAUC) hakijaidhinishwa na TCAA kutoa mafunzo ya urubani kama ambavyo kilikuwa kimeweka matangazo katika tovuti yake. Wanachi wanashauriwa kuchukua tahadhari kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na matangazo kama hayo.





Imetolewa na
Ofisi ya Habari
MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA

Post a Comment

0 Comments