Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Abiria mia moja waliokuwa wasafiri na shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) wakwama jijini DAR.

Zaidi ya abiria mia moja wa ndege ya ATCL wamekwama nchini Tanzania, baada ya safari zao kuahirishwa. 

Wengi wao wakielekea nchini Comoros na wengine wakiwa katika safari za ndani, kuelekea Mtwara na Kigoma wamekwama kwa siku mbili mjini Dar es salaam.

Abiria hao imebidi wakodiwe hoteli kama ilivyo ada wakisubiri muafaka wa namna watakavyosafiri kuelekea Comoro. 

Sababu za kukwama kwa abiria hao inaelezwa kuwa ni kutokana na marubani wa shirika hilo kwenda likizo fupi ya siku kuu za mwisho wa mwaka, na hawajarejea kazini tangu walipo ondoka, ingawa walitegemewa kurejea kazini tarehe 27 mwezi huu, baada ya sherehe za Christimas.

Hivi karibuni, mwezi oktoba, ATCL ilitangaza kusitishwa kidogo kwa huduma zake kutokana na ndege yake pekee aina ya De Havilland Canada DHC-8-Q311 Dash 8, 5H-MWF kuingia katika matengenezo. Mpaka sasa ndege hii bado ipo katika matengenezo katika karakana ya ndege ya ATCL, Dar es salaam.
De Havilland Canada DHC-8-Q311 Dash 8, 5H-MWF
Ndege hii ilikuwa ikihudumiwa na marubani, mafundi na wahudumu wa ndani ya ndege wazawa.

Hata hivyo baada ya Dash 8 kuingia katika matengenezo ATCL iliamua kukodi ndege aina ya Canadian CRJ-200, 5Y-WWA, ambapo imekuwa ikifanya safari katika miji ya Kigoma, Mtwara na Moroni, Comoros. 
Canadian CRJ-200, 5Y-WWA
Ndege hii imekodiwa kutoka Kenya.

Ndege hii ya kukodisha imekuja na marubani wake (wageni) pamoja na baadhi ya wahudumu wa ndani ya ndege kutoka katika shirika linalomiliki ndege hiyo, ikiwa ni miongoni mwa masharti ya ukodiswaji na uendeshwaji wa ndege hiyo.


Mtandao wa BBC unaandika kuwa;

Sharifu Hashim, Balozi wa heshima wa Comoro huko Chicago nchini Marekani, anasema mambo yake mengi yamekwama kutokana na tukio hili na hajapata uhakika ataondoka lini

Zenabal Mwarabu yeye hofu yake ni kwa namna gani ataweza kuiwahi ndege aliyokuwa aunganishe Kisiwani Comoro kuelekea katika kisiwa kingine cha Rarinyo.

Msawi Seifu anasema ijapokuwa tatizo hili limetokea lakini Air Tanzania ni mkombozi kwa wana Comoro.

Hata hivyo Lily Fungamtama, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ATCL amesema tayari Air Tanzania inashughulika kuhakikisha abiria wote wanasafiri mapema kesho.



Post a Comment

0 Comments