Air Tanzania imeainisha
mipango yake ya uendeshaji kwa ndege zake mpya mbili aina ya Dash 8-400s zinazotegemewa
kuwasili katika nusu ya pili ya mwezi ujao.
Gharama zilizolipwa na serikali
ya Tanzania kwa ajili ya manunuzi ya ndege hizo, tayari zilishadokezwa mwezi
Juni na waziri wa fedha na mipango, Dr Phillip Mpango wakati wa kuwasilisha
bungen taarifa juu ya hali ya uchumi nchini Tanzania.
"Serikali itanunua
ndege tatu: Bombardier CS300 moja yenye uwezo wa kubeba hadi abiria 150 na Bombardier
Q400 mbili zenye uwezo wa kubeba abiria hadi 80 kila moja," alinukuliwa
Dkt Mpango.
Hakuna tarehe ya kuwasili
kwa C Series, au uthibitisho wowote kwamba itaagizwa lini kwa ajili ya Air
Tanzania, uliotolewa.
Kaimu mkurugenzi mkuu Patrick
Itule anasema kuwasili kwa Q400 kutaleta mapinduzi makubwa ya upanuzi katika
mtandao wa safari unaomilikiwa na shirika hilo ambapo kwa sasa kuna Kigoma,
Mtwara na Mwanza ndani ya nchi na kikanda ni Moroni, Comoro.
Kwa mujibu wa Itule,
sambamba na ndege pekee ya Air Tanzania inayofanya kazi kwa sasa, Dash 8-300,
hizo Q400 mbili zitatumika hatua kwa hatua kuanza kutoa huduma za safari
kuelekea: Dodoma; Mwanza; Arusha; Mbeya; Tabora; Mpanda; Kilimanjaro; Zanzibar;
Pemba Wawi; na Bukoba.
Hata hivyo, kuimarika tena kwa Air
Tanzania pia kutategemea si tu kuweka sawa madeni yake ambayo
iliripotiwa yanakadiriwa kufikia shilingi billion 93 sawa na dola za kimarekani milioni 50.8, lakini pia idadi kubwa ya wafanyakazi wake wanaokadiriwa
wafanyakazi 200 wakiitumikia ndege moja. Tayari utawala wa rais John Magufuli umeripotiwa
kuteuwa jopo la wataalam watakao pitia na kubuni mpango unaofaa kulirejesha shirika hilo
la ndege linalochechemea katika ubora
wake..
Katika kuonesha nia ya dhati
ya kurejesha Air Tanzania katika sifa yake ya zamani, Waziri wa Kazi, Mawasiliano
na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amemsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Air Tanzania, Johnson Mfinanga, na vile vile Mkurugenzi wa Uendeshaji,
Sadick Muze, kwa kuwa walichagua rubani asiye na sifa/viwango sahihi kwenda
nchini Canada kwa ajili ya mafunzo ya ndege, Q400, katika kampuni ya Bombardier
(Montréal Trudeau).
Nafasi hiyo ya Mkurugenzi
Mtendaji imesha tangazwa kuwa wazi kwa kuajiri hali inayoonesha kuwa bwana
Mfinanga sasa kaondolewa kabisa. Bwana Patrick Itule ndiye anaye kaimu nafasi hiyo kwa sasa.
0 Comments