Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Kenya Airways (KQ) yabadili ndege ya abiria "Dreamliner" kubebea mizigo

Katika hali ya kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi na kuendelea kupambana kwenye biashara katika kipindi hiki cha janga la #COVID-19, shirika la ndege la Kenya, Kenya airways limekuja na ubunifu wa kutumia ndege zake za dreamliners kubeba na kusafirisha mizigo.

Mizigo inayosafirishwa ni misaada ya madawa na vifaa tiba na pia vyakula na mbogamboga.

Mizigo hiyo husafirishwa baina ya Kenya na nchi nyingine. Ndege ya kwanza ya mizigo ilikuwa ni ya madawa na vifaa tiba iliyoondoka Nairobi kuelekea Johannesburg, Afrika ya Kusini.

Ndege ya pili ya mizigo ilibeba mazao ya shambani, mbogamboga kutoka Nairobi ikielekea London Uingereza.



Ndege ya tatu ilikuwa ni ya madawa na vifaa tiba kutoka China kwenda Kenya vikiwa ni katika jitihada za kupambana na janga la #COVID-19.




Kwa kawaida ndege hizi za dreamliner hubeba abiria. Lakini kufuatia kipindi hiki cha janga la  COVID19 mashirika ya ndege yamelazimika kusitisha kutoa huduma za usafiri wa abiria kutokana na makatazo ya mataifa mbalimbali. Hivyo imelazimu makampuni ikiwemo KQ kubadili matumizi ya ndege hizo na hivyo kuendelea kutoa huduma ya kusafirisha mizigo. Ili kuweza kufanya utaratibu huu wa kusafirisha mizigo katika chumba cha ndege ambacho kawaida hukaliwa na abiria (Passenger Cabin) ni lazima kufuata utaratibu na muongozo uliowekwa na mamlaka (CAA) zinazosimamia usafiri wa anga kama vile KCAA, FAA, EASA na TCAA.

Katika makala nyingine tutaangalia taratibu na miongozo inayowezesha kubadili ndege ya kubeba abiria na kuwa ya kubeba mizigo.

Tadhali endelea kutembelea kurasa huu kwa habari zaidi za sekta ya usafiri wa anga na wana anga.

Post a Comment

0 Comments