Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

5H-MZA yaanguka baharini ikiwa na abiria 12 na marubani 2.

Ndege aina ya Cessna 208B yenye usajili 5H-MZA yaanguka baharini huko Comoros ikiwa na watu 14 ndani yake. Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la FLY ZANZIBAR LIMITED ikiwa imekodiwa na shirika la ndege la AB AVIATION la Comoro, ikifanya safari Y61103 kati ya kisiwa cha Moroni na Mohéli, ilianguka wakati ikielekea kutua katika uwanja wa Bander es Salaam Airport, Fomboni, Comoros – katika kisiwa cha Moheli.



Shirika la ndege la AB Aviation lilitangaza kupotea kwa ndege hiyo iliyopaa kutoka Moroni saa tano na dk 50 na kupotea katika radar, baharini, umbali wa 2.5 km kutoka uwanja wa ndege wa Mohéli

Juhudi za utafutaji na uokoaji zinaendelea, mpaka sasa ni baadhi ya mabaki ya ndege tu ndio yamepatikana. Matumaini ya kupata abiria na marubani wakiwa hai yanazidi kufifia.

Taarifa zinaeleza kuwa hivi karibuni kumekuwa na hali mbaya ya hewa baharini katika maeneo ya visiwa vya comoro.


Orodha ya majina ya abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo



Baadhi ya mabaki ya ndge  hiyo yakiwa yameokotwa na wavuvi


Baadhi ya mabaki ya ndge  hiyo yakiwa yameokotwa na wavuvi


Baadhi ya mabaki ya ndge  hiyo yakiwa yameokotwa na wavuvi

Baadhi ya mizigo ya abiria ikiwa imeokotwa na wavuvi


Baadhi ya mizigo ya abiria ikiwa imeokotwa na wavuvi



Taarifa za ndege kwa mujibu wa mtandao:
Namba ya usajili Tanzania: 5H-MZA
Mtengenezaji: PRATT AND WHITNEY CANADA CORP.
Aina: CESSNA 208B Aina za Enjini: PT6A-114A
Tarehe ya Safari yake ya kwanza: 2016
Kampuni miliki/muendeshaji : FLY ZANZIBAR LIMITED, P O BOX 3648 ZANZIBAR
Tarehe ya Kusajiliwa Tanzania: 29/01/2022

Taarifa zaidi kuhusu ajali hii zitawajia kadri zinavyotufikia. Tunatoa pole nyingi sana kwa ndugu na jamaa wa abiria na marubani waliokutwa na ajali hii.

Post a Comment

0 Comments