Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Air Tanzania kununua ndege nne aina ya Bombardier Q400.

  • Yasaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya Bombardier ya Canada
  • Ndege ya kwanza kati ya ndege hizo inatarajiwa kuwasili hapa nchini mwishoni mwa mwaka huu wa 2014.

Mkataba wa makubaliano ya awali ya ununuzi wa ndege hizo umetiwa saini jijini Dar es salaam, jumanne tarehe 19/08/2014, kati ya kaimu mkurugenzi mkuu wa ATCL capt Milton John Lazaro na Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni hiyo ya Bombardier kanda ya Afrika.

Kapteni Milton amesema ndege hizo zenye mwendo wa kasi zina uwezo wa  kuchukua hadi abiria themanini (80) kila moja kwa wakati mmoja na ndege ya kwanza kati ya ndege hizo inatarajiwa kuwasili hapa nchini mwishoni mwa mwaka huu wa 2014.

"Ni ndege ambayo pia inatumika na nchi jirani na zingine kimataifa, ni ndege yenye mwendo wa kasi amabayo uwezo wake wa kuruka, kasi yake unakaribiana na ndege aina ya jet. Kwa hiyo ni ndege ambayo sisi kwetu katika mchakato wa kuimarisha kampuni itatuletea mafanikio makubwa na faida kubwa" alisema kapteni Lazaro.

Uchunguzi wa mtandao huu wa aviationtz.com umegundua kuwa ndege hizi hutumiwa na shirika la ndege la Ethiopian Airways na pia shirika la ndege la Malawian Airlines ambao walipewa ndege hiyo kutoka Ethiopian Airways na ndege hizi zimekuwa zikifanya safari zake kutoka Ethiopia mpaka hapa Dar es salaam na pia kutoka Malawi na kuja hapa Dar es salaam.

Ndege aina ya Q400 ya Ethiopian Airways.


Ndege aina ya Q400 ya Malawian Airways.
Aviationtz kama wadau wa sekta hii ya usafiri wa naga tunasubiri kwa hamu kubwa ujio wa ndege hizi, na itakuwa ni faraja kubwa kwetu na watanzania kwa ujumla kwani italeta maendeleo katika sekta hii na kuzidi pia kuliimarisha shirika letu la ATCL.

Bombardier ni kampuni pekee duniani inayotengeneza ndege na treni za kisasa kwa pamoja. Makao makuu ya kampuni hii yapo Montréal, Canada. Miongoni mwa ndege zinazotengenezwa na kampuni hii ni Q-SeriesCSeries na CRJ Series.

Air Tanzania (ATCL) ni shirika la ndege la Taifa la Tanzania (National Carrier). Lilianzishwa machi 11,1977 baada ya kuvunjika lililokuwa shirika la ndege la Afrika Mashariki, East African Airways (EAA). Kwa sasa shirika hili lina ndege moja tu aina ya Dash 8, Q300. 

Ukipenda kufahamu historia ya ATCL tembelea mtandao huu..http://www.angelfire.com/falcon/african/airtanzania.html

Post a Comment

1 Comments

  1. I wonder whether they will consider hiring/training all the idle TZ pilots !!!

    ReplyDelete