Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Hivi,Umeshawahi kufikiria/kushuhudia jinsi ajali za ndege zinavyotisha?

Ajali za ndege zimekuwa zikitokea mara chache sana ukilinganisha na ajali za vyombo vingine vya usafiri kama vile magari, treni pikipiki n.k. Hii ni kutokana na udhibiti wa hali ya juu kutoka kwa mamlaka zinazohusika na kusimamia utengenezaji na uendeshaji wa vyombo vya angani, ambapo kwa hapa kwetu mamlaka husika ni Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA).
TCAA ni miongoni mwa mamlaka zenye nguvu kiutendaji hali iliyopelekea kutambulika na mamlaka zingine duniani kwa usimamizi wake thabiti wa usalama wa safari za angani hapa Tanzania.

Anga la Tanzania ni salama kwa safari za ndege na ndio maana mashirika makubwa ya ndege duniani kama vile Qatar, Emirates, KLM, Air France, Oman air, Ethiopian airlines, Flydubai, Etihad, KQ n.k yanafanya safari zao kuja hapa Tanzania.

Pamoja na kuwa ajali za ndege huwa hutokea chache lakini madhara yake huwa ni makuwa sana na pengine kushinda hata ajali za vyombo vingine. Hii ni kutokana na ukweli kwamba nyingi ya ajali za ndege hupelekea watu wote wanaokuwepo katika chombo husika kupoteza maisha.

Mfano wa ajali mbaya ya ndege kuwahi kutokea ni ajali ya ndege ya shirika la ndege la Msumbiji, LAM Airlines, aina ya Embrear 190 iliyotengenezwa oktoba 2012. Ajali hii ilitokea tarehe 29/11/2013, ambapo ndege hiyo yenye usajili C9-EMC ilikuwa ikifanya safari namba 470  kutoka Maputo, Msumbiji kuelekea Luanda, Angola. Ndege hii ikiwa na abiria 27, marubani 2, wahudumu 3 pamoja na fundi 1, ilianguka nchini Namibia katika mbuga ya hifadhi ya wanyama ya Bwabwata. Watu wote 33 waliokuwepo katika ndege hiyo walipoteza maisha palepale ambapo ndege iliungua yote na kubaki majivu.

Taarifa za uchunguzi wa ajali hii zilionesha kuwa rubani aliidondosha ndege hii kwa makusudi.

Iwapo utapenda kujua zaidi juu ya nini kilichotokea, na kwanini rubani akaamua kuidondosha ndege hii, basi tupatie maoni yako nasi tutakujuza zaidi.

Tazama picha zifuatazo za moja ya ajali ya ndege ya LAM Airlines.






Post a Comment

1 Comments