Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

AJALI YA NDEGE 5H-FZS CESSNA 182G SKYLANE

Ndege aina ya  Cessna 182G Skylane C/N 182-66371 yenye usajili 5H-FZS imeanguka leo 18/5/2023 majira ya saa tano na nusu wakati ikiruka katika kiwanja cha ndege Matambwe katika hifadhi ya taifa Nyerere.


Ndege hiyo imepata ajali ikiwa imebeba watu wane (4) ambao ni rubani mmoja (1) na abiria watatau (3) ambao ni askari uhifadhi wanayama pori na wakiwa wanaenda kwenye doria.

Kwa mujibu wa taarifa, katika ajali hiyo watu wawili akiwemo rubani wamefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa na kukimbizwa zahanati kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza, na kisha kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa mtandao wa mamlaka ya usafiri wa anga hapa nchini, ndege hiyo yenye usajili 5H-FZS imesajiliwa chini mwaka 2021 ya umiliki wa taasisi ya Frankfurt Zoological Society.

Picha ya 5H-FZS ilivyokuwa nzima, picha hii ilipigwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Es Salaam. (Picha kwa hisani ya mtandao wa airport-data)

Endelea kutembelea kurasa zetu za mitandao ili kupata taarifa zaidi.


Post a Comment

0 Comments