![]() |
Paris - Ufaransa imepitisha sheria ya kupiga marufuku baadhi ya safari za ndege za ndani na kuwahimiza wasafiri kuchukua treni badala yake. Chini ya sheria mpya, safari za ndege ambazo zinaweza kubadilishwa na safari ya treni ya chini ya saa mbili na nusu zinapaswa kufutwa.
Usafiri wa ndege kati ya Paris na vituo vya kikanda kama vile Nantes, Lyon na Bordeaux sasa utapigwa marufuku.
Safari za ndege za kuunganisha hazijaathiriwa.
Sheria
hiyo imeanza kutumika rasmi siku ya jumanne wiki iliyopita ikiwa ni miaka miwili toka wabunge
wapige kura ya kusitisha
njia ambapo safari za ndege zinaweza kufanywa kwa treni ndani ya saa mbili na
nusu. Lengo la sheria hiyo ni kupunguza utoaji wa hewa ukaa (CO2).
Hata
hivyo, shirika la ndege la kitaifa la Ufaransa lilikuwa tayari limeshatsitisha safari
katika njia tatu ambazo zilizingatiwa kuwa nyingi sana kutokana na utoaji wa
hewa ukaa (CO2). Safari zote tatu zilitoka uwanja wa ndege wa pili wa Paris,
Orly, zikihudumia miji ya Bordeaux, Lyon na Nantes. Miji hiyo mitatu yote iko
kwenye mtandao mpana wa reli ya kasi ya juu nchini Ufaransa, na kuchukua treni
pia ni haraka zaidi kuliko kuruka kwa ndege.
Air France ilikubali kuacha njia hizo za moja kwa moja ili kupata usaidizi wa kifedha wa coronavirus kutoka kwa serikali ya ufaransa mnamo 2020.
![]() |
Miji iliyoathirika na katazo la safari za masafa mafupi ndani ya Ufaransa |
Sheria inabainisha huduma za treni katika njia zilizoathirika na katazo hili lazima ziwe za mara kwa mara, kwa wakati na ziunganishwe vyema ili kukidhi mahitaji ya abiria ambao wangesafiri kwa ndege - na kuweza kustahimili ongezeko la idadi ya abiria.
Hatua
hiyo inajiri huku wanasiasa wa Ufaransa pia wakijadiliana jinsi ya kupunguza
hewa chafu kutoka kwa ndege za kibinafsi.
0 Comments