Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAA YASIMAMISHA BOEING 737 MAX 9 KUPISHA UKAGUZI WA KIUFUNDI, WA DHARURA.



Mamia ya safari zaaghirishwa na maelfu ya wasafiri kuathirika.

Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa anga ya Marekani, FAA, imeamuru kusimamishwa na kufanyiwa "ukaguzi wa haraka" kwa ndege za Boeing B737 Max 9. Agizo hilo linakuja baada ya mlango wa dharura wa B737 Max 9 ya Alaska Airlines kuchomoka wakati ndege ya Alaska Airlines ikiwa angani, na kuacha shimo kwenye ubavu wa ndege. Ndege ilitua salama bila majeraha makubwa. 

Inakadiriwa jumla ya ndege takriban 171 duniani kote zitaathiriwa na agizo hili. 

Kampuni hiyo kubwa ya uundaji ndege ya Marekani iko chini ya uangalizi mkali kuhusu usalama wa ndege yake maarufu ya B737 Max 9. Boeing ilisema ilikaribisha uamuzi wa FAA, na kuongeza timu zake ziliwasiliana kwa karibu na mdhibiti (FAA).

Sehemu kubwa ya ndege zilizoathiriwa zinamilikiwa na mashirika ya ndege ya Marekani. 

United Airlines imesimamisha ndege zake zote 79 za Max 9.

Pichani ni ndege B737 Max 9 ya Alaska Airlines iliyopata tatizo la mlango wa dharura kuchomoka ndege ilipokuwa angani.

Alaska Airlines ilisema ilighairi safari 160 za ndege siku ya Jumamosi, na kuathiri takriban abiria 23,000.

Mashirika mengine ya ndege ambayo pia yanaendesha ndege hizo yameziondoa kazini kwa muda.

Wakala wa Usalama wa Anga wa Umoja wa Ulaya (EASA) unafuata agizo la FAA, lakini usumbufu wa safari za ndege katika bara hilo unatarajiwa kuwa mdogo. EASA ilisema inaamini kuwa hakuna mashirika ya ndege ya Ulaya yanayotumia Max 9 yenye usanidi (configuration) unaosimamiwa na agizo la FAA.

Mdhibiti wa Uingereza wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (CAA) alisema hakuna ndege za Boeing 737 Max 9 zilizosajiliwa nchini Uingereza na kwa hivyo athari itakuwa "ndogo".

"Tumewaandikia wachukuzi wote wa vibali wasio wa Uingereza na wa kigeni kuomba uthibitisho kwamba ukaguzi umefanywa kabla ya operesheni yoyote katika anga ya Uingereza," msemaji wa CAA alisema.

Shirika la ndege la Turkish Airlines limesitisha safari zake tano kati ya 737 Max 9.

Flydubai ilisema 737 Max 9 zake tatu hazikuathiriwa kwa vile zilikuwa na "usanidi tofauti" ikilinganishwa na ndege za Alaska Airlines. 

Air Tanzania nayo inamiliki B737 Max 9 moja.

Endelea kufuatilia ukurasa huu na mitandao mingine ya @aviationtanzania kwa taarifa zaidi za masuala ya usafiri wa anga.

#aviationtanzania✈️ #b737max9 #faa #alaskaairlines

Post a Comment

0 Comments