Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Air Tanzania kuanza safari za Pemba mwezi machi.

Shirika la ndege la Air Tanzania limetangaza kuanza safari za Pemba kuanzia tarehe 6 mwezi ujao. Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, ATCL imetoa tangazo likieleza kuwa safari za kuelekea Pemba zitakuwa ni mara tatu kwa wiki, zikifanyika katika siku za Jumatano, Ijumaa na Jumapili.



Shirika hilo limetangaza nauli kuwa kama ifuatavyo;

Dar - Pemba TZS 229,000 kwenda tu.

Zanzibar - Pemba TZS 157,000 kwenda tu.

Tiketi za safari zinapatikana kupitia tovuti www.airtanzania.com au kupitia app ya Air Tanzania inayopatikana play store na app store.

Safari hizi za Pemba zinakuja ikiwa ni siku chache tu mara baada ya shirka hili kutangaza kuanza kwa safari zake za Dubai zinazotarajiwa kuanza rasmi tarehe 31 Machi 2024, ambapo zitafanyika mara nne (4) kwa wiki, zikifanyika kila Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili. Nauli ya kutoka DAR - Dubai ikianzia dola za Marekani 530. ($530).



Air Tanzania Company Limited (ATCL) ni shirika la ndege linalomilikiwa na serikali ya Tanzania lenye idadi ya jumla ya ndege 14; Dash 8-Q300 moja, Dash 8-Q400 tano, Airbus A220-300 nne, Boeing 737 Max 9 moja, Boeing 787-8 Dreamliner mbili na Boeing 767-300F moja (Cargo Freighter). Kufikia mwisho wa 2024, shirika hili linatarajia kuongeza ndege idadi ya ndege zake, ambapo linatarajiwa kupokea ndege nyingine mbili; Boeing 737 Max 9 moja na Boeing 787-8 Dreamliner moja.

Makao makuu ya ATCL yapo jijini Dar Es Salaam. Na kitovu chake cha undeshaji/biashara ni Julius Nyerere International Airport.


Post a Comment

0 Comments