Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Air Tanzania yapokea ndege mpya aina ya Boeing 737 MAX 9. Hii inakuwa ndege ya pili aina ya Boeing 737 MAX 9 kwa Air Tanzania.

Ndege mpya ya Air Tanzania, aina ya Boeing 737 MAX 9 iliyosajiliwa kwa namba 5H-TCQ, na kubatizwa “Ruaha National Park”, inatarajiwa kuwasili hapa nchini siku ya jumanne, tarehe 26 Machi 2024 katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere

Pichani ni B737 MAX 9, 5H-TCQ ya Air Tanzania ikipaa kutoka katika uwanja wa ndege wa San Juan Luis Muñoz Marín International (SJU / TJSJ), Puerto Rico. (Picha kwa hisani ya David @aviation_finders )

5H-TCQ, Boeing 737 MAX 9 ni ndege ya pili kati ya mbili aina hizo zilizoagizwa (kununuliwa) na serikali ya Tanzania moja kwa moja kutoka Boeing. Tarehe 3 Oktoba 2023 Air Tanzania ilipokea Boeing 737 MAX 9 ya kwanza iliyosajiliwa kwa namba 5H-TCP, na kubatizwa “Olduvai Gorge”.

5H-TCQ “Ruaha National Park” imeondoka tarehe 23 Machi 2024 ikibeba safari namba TC300, kutoka Seattle (BFI) nchini Marekani kwa safari yake ya kuja Tanzania. Itapitia katika miji ya San Juan (SJU) nchini Puerto Rico, na Dakar (DSS) nchini Senegal, kwa mapumziko na huduma za kiufundi na hatimaye kuingia anga la Tanzania siku ya tarehe 26 Machi 2024, na kupokelewa katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Tembelea kurasa zetu za mitandao ya kijamii kwa taarifa zaidi @aviationtanzania

@airtanzania_atcl @boeing

#aviationtanzania #aviationtanzanianews #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatanews #airtanzania #airtanzania737 #airtanzania737max #airtanzania737max9 #boeing #boeing737 #737max #737max9 #aviation #aviationdaily #aviationgeek #aviationphotography #planespotting #planepictures #tanzania #boeinglovers #aviationlovers #tanzania

Post a Comment

0 Comments